top of page
Search

Announcement

UONGOZI WA SHULE YA SEKONDARI LOYOLA (SHULE YA

KIKATOLIKI UNAPOKEA WANAFUNZI WA MADHEHEBU NA

JINSIA ZOTE) UNAPENDA KUWATANGAZIA WAZAZI/WALEZI NA

WANAFUNZI KUWA FOMU ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA

KWANZA, KIDATO CHA PILI NA KIDATO CHA TATU 2023. PIA

NAFASI ZA KUJIUNGA NA KIDATO CHA TANO 2022/2023 BADO

ZIPO. FOMU ZOTE ZINAPATIKANA:-

  • LOYOLA HIGH SCHOOL

  • TOVUTI YA SHULE (www.loyola.ac.tz )

  • MSIMBAZI CENTRE:

Chumba Na. 09 Imani Stationery.

Umoja wa Mashule Chumba Na. 22

Chumba Na. 19


GHARAMA ZA FOMU

1. KIDATO CHA KWANZA TSHS 20,000/=

2. KIDATO CHA PILI NA KIDATO CHA TATU TSHS. 30,000/=

3. KIDATO CHA TANO 2022/2023 TSHS. 20,000/=


Pia malipo ya fomu yanaweza kufanywa shuleni au kwenye Akaunti ya shule; tawi lolote la NBC

Akaunti Namba 022101000890 au CRDB Akaunti Namba 0150315988100, Jina la Akaunti:

LOYOLA HIGH SCHOOL, karatasi ya malipo (bank pay-in-slip) iambatanishwe na fomu ya

kujiunga kwa uthibitisho zaidi. Fomu haitapokelewa bila risiti (bank pay-in-slip) ya malipo ya

fomu ya kujiunga.


TAREHE YA USAHILI

Kidato cha Kwanza:

Mtihani wa Kwanza wa Usahili - Ijumaa, 14 Oktoba 2022

Mtihani wa Pili wa Usahili - Jumamosi, 22 Oktoba 2022

Kidato cha Pili na Kidato cha Tatu - Jumatano 14 Desemba, 2022


MUDA WA KAZI

Kuanzia saa 2.00 Asubuhi hadi saa 10.00 jioni siku za Jumatatu mpaka Ijumaa.


MAHALI ILIPO SHULE

Shule ya Loyola iko eneo la Mabibo Farasi, kama kilometa 10 kutoka Magharibi mwa Jiji la

Dar es Salaam. Shule iko katikati ya barabara kuu mbili Mandela na Morogoro. Lango kuu la

shule liko katika Barabara ya Kigogo (Old Morogoro Road). Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi

muda wa kazi simu namba: 0769-844812, 0785-805115, 0658-233088


TANGAZO LA KUJIUNGA NA MASOMO 2023 (1)
.pdf
Download PDF • 623KB

bottom of page