top of page
Search

Nafasi za kujiunga na kidato cha Tano 2023

Uongozi wa shule ya Sekondari Loyola inayomilikiwa na Mapadre wa Shirika la Yesu (Majesuit) unapenda kuwatangazia wazazi/walezi na wanafunzi nafasi za kujiunga na masomo Kidato cha Tano 2023. Shule inapokea wanafunzi wa madhehebu na jinsia zote. Shule ni ya bweni kwa wasichana na kutwa kwa wavulana.


Fomu za kujiunga zinapatikana kwa gharama ya Tshs. 20,000/= katika shule ya Sekondari ya Loyola, Msimbazi Centre chumba namba 009 (Imani Stationery), chumba namba 19, Umoja wa shule Chumba namba 22, Parokia ya K/Ndege Dodoma, Parokia ya Nyakahoja Mwanza, Notre Dame Schools, Temdo, Njiro na katika tovuti ya Shule www.loyola.ac.tz.


Malipo ya fomu yafanyike kwenye Akaunti ya shule; tawi la CRDB Akaunti Namba 0150315988101 Jina la Akaunti: LOYOLA HIGH SCHOOL. Karatasi ya malipo (bank pay-inslip) iambatanishwe na fomu ya kujiunga kwa uthibitisho zaidi. Fomu haitapokelewa bila risiti (bank pay-in-slip) ya malipo ya fomu ya kujiunga.


TAREHE YA USAILI - DAR ES SALAAM SHULE YA SEKONDARI LOYOLA

  1. Mtihani wa usaili wa kwanza Ijumaa tarehe 10 Februari 2023.

  2. Mtihani wa usaili wa pili Jumamosi tarehe 18 Februari 2023.

  3. Mtihani wa usaili wa tatu Jumamosi tarehe 25 Februari 2023.


MIKOANI: USAILI UTAFANYIKA JUMAMOSI TAREHE 18 FEBRUARI 2023 TU

  1. Mwanza mtihani wa usaili utafanyikia Parokia ya Nyakahoja.

  2. Dodoma mtihani wa usaili utafanyikia shule ya Msingi Mt. Inyasi.

  3. Arusha na Moshi mtihani utafanyikia Notre Dame Schools, Temdo, Njiro.


MUDA WA KAZI

Kuanzia Saa mbili kamili Asubuhi hadi saa tisa kamili Alasiri siku za Jumatatu mpaka Ijumaa.


Shule inatoa michepuo ifuatayo

  • ECA - (Economics, Commerce and Accountancy)

  • EGM - (Economics, Geography and Mathematics)

  • HGE - (History, Geography and Economics)

  • HGK - (History, Geography and Kiswahili)

  • HGL - (History, Geography and English Language)

  • HKL - (History, Kiswahili and English Language)

  • PCB - (Physics, Chemistry and Biology)

  • PCM - (Physics, Chemistry and Mathematics)

  • PMC - (Physics, Mathematics and Computer Science)

  • PGM - (Physics, Geography and Mathematics)

  • CBG - (Chemistry, Biology and Geography)

MAHALI ILIPO SHULE

Shule ya Loyola iko eneo la Mabibo Farasi, kama kilometa 10 kutoka Magharibi mwa Jiji la Dar es Salaam. Shule iko katikati ya barabara kuu mbili Mandela na Morogoro. Lango kuu la shule liko katika Barabara ya Kigogo. Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi muda wa kazi

simu namba: 0769-844812, 0785-805115, 0658-233088


bottom of page